naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 3

Majukumu ya watoto yanapaswa kuzingatia mambo gani?

From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma

Kwa kweli, si jambo la mjadala kuwa jamii ina jukumu la kumlea mtoto. Hata hivyo, mtoto naye ana majukumu anuwai anayopaswa kuyatekeleza katika jamii yake. Mtoto anaposaidiwa, haifai ajipakatie mikono. Afanye juhudi kutekeleza majukumu yake ili anayemsaidia awe na sababu ya kuendelea kumsaidia. Vile vile, majukumu kwa mtoto yanapaswa kuzingatia hali na umri wake.
Watoto wanapaswa kujiunga na shule kwa wakati ufaao na kuendelea na masomo hadi watakapohitimu kiwango kinachostahili. Shuleni, watoto hawana budi kutii na kuzingatia masomo. Hili litamsaidia kupata stadi, ujuzi, maarifa, maadili na mielekeo inayofaa maishani.
Mtoto anapaswa kuwasaidia wazazi wake na kufanya kazi ndogo ndogo kulingana na umri wake. Anapofanya kazi hizo anapaswa kuwajibikia vifaa anavyotumia. Hii itamsaidia kuwa na uwajibikaji katika maisha yake.
Mbali na hayo, mtoto anapaswa kushirikiana na wenzake shuleni na hata katika jamii. Ashirikiane na wenzake katika ujifunzaji. Anapofanya hivyo, awe makini kuwateua marafiki wazuri. Mmoja akifanya jambo lisilofaa, amshauri abadilike; akishindwa, amwombe mwalimu msaada. Kwa kufanya hivyo, atakuwa amemsaidia mwenzake.

Majukumu ya watoto yanapaswa kuzingatia mambo gani?

  1. AAfya na uwezo wao shuleni.
  2. BElimu na kimo chao.
  3. CUmri na hali zao.
  4. DMaadili na maarifa yao.

Answer

C. Umri na hali zao.

Kifungu kinataja moja kwa moja hali na umri wa mtoto.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test