naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 6

Watu wanashauriwa kufanya nini ili kusaidia kupambana na kifua kikuu?

From Test 13 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Kifungu cha Ufahamu
Kifuakikuu ni ugonjwa ambukizi. Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na aina tofauti za bakteria. Kwa kawaida huathiri mapafu, vilevile huweza kuathiri sehemu nyingine za mwili. Kifuakikuu huambukizwa kutoka kwa mgonjwa hadi mtu mwingine. Njia kuu ya maambukizi ni kupitia hewa hasa wakati mgonjwa anapokohoa, kupiga chafya au kutema mate.

Dalili za kawaida za maambukizi ya kifuakikuu ni kikohozi sugu, kukohoa damu, homa, kutokwa na jasho usiku na kukonda. Tiba ya ugonjwa wa kifuakikuu ni pamoja na kupewa tembe za kumeza na kudungwa sindano.

Uhamasishaji wa kijamii pia ni muhimu katika kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu. Watu hushauriwa wakubali kupimwa hali zao za kiafya kila mara na kupewa chanjo kuzuia kupata kifua kikuu.

Watu wanashauriwa kufanya nini ili kusaidia kupambana na kifua kikuu?

  1. AKujiepusha na elimu ya afya
  2. BKupata chanjo na kuhimiza wengine wapimwe
  3. CKuficha ugonjwa wao
  4. DKunywa maji mengi

Answer

B. Kupata chanjo na kuhimiza wengine wapimwe

Kifungu kinasema watu hushauriwa "wakubali kupimwa hali zao za kiafya kila mara na kupewa chanjo."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test