naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 7

Ni ujumbe gani muhimu mwandishi anawasilisha katika kifungu hiki?

From Test 13 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Kifungu cha Ufahamu
Kifuakikuu ni ugonjwa ambukizi. Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na aina tofauti za bakteria. Kwa kawaida huathiri mapafu, vilevile huweza kuathiri sehemu nyingine za mwili. Kifuakikuu huambukizwa kutoka kwa mgonjwa hadi mtu mwingine. Njia kuu ya maambukizi ni kupitia hewa hasa wakati mgonjwa anapokohoa, kupiga chafya au kutema mate.

Dalili za kawaida za maambukizi ya kifuakikuu ni kikohozi sugu, kukohoa damu, homa, kutokwa na jasho usiku na kukonda. Tiba ya ugonjwa wa kifuakikuu ni pamoja na kupewa tembe za kumeza na kudungwa sindano.

Uhamasishaji wa kijamii pia ni muhimu katika kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu. Watu hushauriwa wakubali kupimwa hali zao za kiafya kila mara na kupewa chanjo kuzuia kupata kifua kikuu.

Ni ujumbe gani muhimu mwandishi anawasilisha katika kifungu hiki?

  1. AJinsi ya kupona kifua kikuu
  2. BAdhari za kifua kikuu
  3. CUgonjwa ambukizi
  4. DUgonjwa wa kifua kikuu

Answer

D. Ugonjwa wa kifua kikuu

Kifungu kizima kinaeleza kwa ujumla kifua kikuu ni nini, kinavyoambukizwa, dalili zake, tiba na uzuiaji wake, hivyo ujumbe mkuu ni kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu wenyewe.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test