CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5
Kifua kikuu kinaweza kuzuiliwa kwa
From Test 13 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Kifungu cha Ufahamu
Kifuakikuu ni ugonjwa ambukizi. Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na aina tofauti za bakteria. Kwa kawaida huathiri mapafu, vilevile huweza kuathiri sehemu nyingine za mwili. Kifuakikuu huambukizwa kutoka kwa mgonjwa hadi mtu mwingine. Njia kuu ya maambukizi ni kupitia hewa hasa wakati mgonjwa anapokohoa, kupiga chafya au kutema mate.
Dalili za kawaida za maambukizi ya kifuakikuu ni kikohozi sugu, kukohoa damu, homa, kutokwa na jasho usiku na kukonda. Tiba ya ugonjwa wa kifuakikuu ni pamoja na kupewa tembe za kumeza na kudungwa sindano.
Uhamasishaji wa kijamii pia ni muhimu katika kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu. Watu hushauriwa wakubali kupimwa hali zao za kiafya kila mara na kupewa chanjo kuzuia kupata kifua kikuu.

- Akufunika mdomo wakati wa kukohoa
- Bkula vyakula baridi
- Ckunywa maji mengi
- Dkukaa ndani ya nyumba
Answer
A. kufunika mdomo wakati wa kukohoa
Kwa kuwa ugonjwa huambukizwa hewani wakati wa kukohoa au kupiga chafya, kufunika mdomo wakati huo husaidia kuzuia maambukizi.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Watu wanashauriwa kufanya nini ili kusaidia kupambana na kifua kikuu?Question 6
- Ni ujumbe gani muhimu mwandishi anawasilisha katika kifungu hiki?Question 7
- Shairi hili linazungumzia nini?Question 8
- Mwandishi anashauri wanafunzi wafanye nini?Question 9
- Kulingana na shairi, elimu hutoa nini?Question 10
- Wazazi wanahimizwa kufanya nini?Question 11