CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 3
Ni mwanafunzi yupi aliyemkatiza mwalimu alipokuwa akiongea?
From Kiswahili — Monitoring Learners Progress 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mwalimu na wanafunzi wanajadiliana kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira)
Mwalimu: Hamjambo wanafunzi?
Wanafunzi: (Wakiamka sawia) Hatujambo mwalimu, shikamoo.
Mwalimu: Marahaba. (Anawaashiria wakae. Wote wanaketi na kushukuru.) Naam, leo ningependa tuzungumze kuhusu namna na umuhimu wa kuyatunza mazingira kwa hivyo…
Matayo: (Anaunyanyua mkono wake) Samahani mwalimu, mazingira ni nini?
Mwalimu: (Akitabasamu) Matayo huishi vituko! Ndilo nililotaka kueleza. Mazingira ni yale yote yanayotuzunguka. Hebu pendekezeni njia mbalimbali za kuyatunza mazingira.
Manyanga: Nadhani ni vyema kukata nyasi ndefu ili kuharibu makao ya mbu.
Kaisari: Ni vyema pia kutunza vyanzo vya maji kama vile mito, chemichemi, mabwawa na maziwa.
Pendo: Nikiongezea, si vyema kutumia mbolea nyingi zaidi hasa za madukani ili tusiyaathiri maji na udongo.
Mwalimu: Nimefurahia michango yenu. Zipo njia nyingi za kuyatunza mazingira. Kimsingi, umuhimu wa kuyatunza mazingira ni kuwafanya viumbe waishi maisha salama.
3. Ni mwanafunzi yupi aliyemkatiza mwalimu alipokuwa akiongea?
- AManyanga
- BMatayo
- CKaisari
- DPendo
Answer
B. Matayo
Matayo aliuliza "mazingira ni nini?" mwalimu akiongea.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Kulingana na mazungumzo haya, yote yanayotuzunguka ndiyoQuestion 4
- Mwishoni, mwalimu alifurahishwa na nini?Question 5
- Binadamu wana mambo mengi wanayoweza kujifunza kutoka kwaQuestion 6
- Kulingana na ufahamu, chakula kitamu kuliko vyote ulimwenguni niQuestion 7
- Nyuki huweza kuwaangamiza watu au wanyama iwapoQuestion 8
- Nyuki hufanya kazi hata wakati wa jua na baridi kutokana na nini?Question 9