CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 2
Ili kuonyesha heshima kuu, mwalimu alipowaamkia, wanafunzi wote
From Kiswahili — Monitoring Learners Progress 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mwalimu na wanafunzi wanajadiliana kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira)
Mwalimu: Hamjambo wanafunzi?
Wanafunzi: (Wakiamka sawia) Hatujambo mwalimu, shikamoo.
Mwalimu: Marahaba. (Anawaashiria wakae. Wote wanaketi na kushukuru.) Naam, leo ningependa tuzungumze kuhusu namna na umuhimu wa kuyatunza mazingira kwa hivyo…
Matayo: (Anaunyanyua mkono wake) Samahani mwalimu, mazingira ni nini?
Mwalimu: (Akitabasamu) Matayo huishi vituko! Ndilo nililotaka kueleza. Mazingira ni yale yote yanayotuzunguka. Hebu pendekezeni njia mbalimbali za kuyatunza mazingira.
Manyanga: Nadhani ni vyema kukata nyasi ndefu ili kuharibu makao ya mbu.
Kaisari: Ni vyema pia kutunza vyanzo vya maji kama vile mito, chemichemi, mabwawa na maziwa.
Pendo: Nikiongezea, si vyema kutumia mbolea nyingi zaidi hasa za madukani ili tusiyaathiri maji na udongo.
Mwalimu: Nimefurahia michango yenu. Zipo njia nyingi za kuyatunza mazingira. Kimsingi, umuhimu wa kuyatunza mazingira ni kuwafanya viumbe waishi maisha salama.
2. Ili kuonyesha heshima kuu, mwalimu alipowaamkia, wanafunzi wote
- Awalisimama ili kupokea salamu yake
- Bwalitaka kujua maana ya majadiliano
- Cwalitaka kujua maana ya mazingira
- Dwalitaja umuhimu wa kuishi katika mazingira safi
Answer
A. walisimama ili kupokea salamu yake
"(Wakiamka sawia) Hatujambo mwalimu, shikamoo."
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Ni mwanafunzi yupi aliyemkatiza mwalimu alipokuwa akiongea?Question 3
- Kulingana na mazungumzo haya, yote yanayotuzunguka ndiyoQuestion 4
- Mwishoni, mwalimu alifurahishwa na nini?Question 5
- Binadamu wana mambo mengi wanayoweza kujifunza kutoka kwaQuestion 6
- Kulingana na ufahamu, chakula kitamu kuliko vyote ulimwenguni niQuestion 7
- Nyuki huweza kuwaangamiza watu au wanyama iwapoQuestion 8