naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 1

Mazungumzo haya yaliandaliwa majira ya saa ngapi?

From Kiswahili — Monitoring Learners Progress 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mwalimu na wanafunzi wanajadiliana kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira)
Mwalimu: Hamjambo wanafunzi?
Wanafunzi: (Wakiamka sawia) Hatujambo mwalimu, shikamoo.
Mwalimu: Marahaba. (Anawaashiria wakae. Wote wanaketi na kushukuru.) Naam, leo ningependa tuzungumze kuhusu namna na umuhimu wa kuyatunza mazingira kwa hivyo…
Matayo: (Anaunyanyua mkono wake) Samahani mwalimu, mazingira ni nini?
Mwalimu: (Akitabasamu) Matayo huishi vituko! Ndilo nililotaka kueleza. Mazingira ni yale yote yanayotuzunguka. Hebu pendekezeni njia mbalimbali za kuyatunza mazingira.
Manyanga: Nadhani ni vyema kukata nyasi ndefu ili kuharibu makao ya mbu.
Kaisari: Ni vyema pia kutunza vyanzo vya maji kama vile mito, chemichemi, mabwawa na maziwa.
Pendo: Nikiongezea, si vyema kutumia mbolea nyingi zaidi hasa za madukani ili tusiyaathiri maji na udongo.
Mwalimu: Nimefurahia michango yenu. Zipo njia nyingi za kuyatunza mazingira. Kimsingi, umuhimu wa kuyatunza mazingira ni kuwafanya viumbe waishi maisha salama.

1. Mazungumzo haya yaliandaliwa majira ya saa ngapi?

  1. ASaa sita adhuhuri
  2. BSaa mbili asubuhi
  3. CSaa kumi jioni
  4. DHatujaelezwa

Answer

D. Hatujaelezwa

Mazungumzo hayataji saa yoyote.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test