naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 15

Ni faida gani ya kutumia vifaa vya mapambo kama herini?

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 8) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ya 13 hadi 15.
Mapambo ya urembo ni vitu au mbinu zinazotumika kuboresha au kurembesha mwonekano wa mtu. Matumizi yao hutofautiana kutoka tamaduni moja hadi nyingine na kwa mtu binafsi. Baadhi ya mapambo ya urembo ni pamoja na vipodozi kama kidomwa, maskara na kivuli cha macho, vito vya mapambo kama pete, herini na mikufu, pamoja na kusuka nywele, kupaka hina na kucha za bandia. Mapambo ya urembo yanaweza kutumiwa kwa madhumuni ya kujiongezea uzuri, kujieleza au hata kuashiria hadhi au utambulisho wa kitamaduni. Hata hivyo, ni muhimu kutumia mapambo haya kwa busara ili kuhakikisha afya na ustawi wa ngozi na mwili kwa ujumla.

15. Ni faida gani ya kutumia vifaa vya mapambo kama herini?

  1. AKupunguza shinikizo la damu.
  2. BKuongeza uzito wa masikio.
  3. CKuongeza urembo wa uso.
  4. DKupunguza maumivu ya kichwa.

Answer

C. Kuongeza urembo wa uso.

Herini huongeza urembo.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test