CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 9
Sentensi iliyopigiwa mstari ni fani gani ya lugha. "Katika masomo, alikuwa wembe."
From Kiswahili — Assessment 2025 (Set 7) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 10.
Bendera alizaliwa yapata miongo miwili iliyopita. Alikuwa mwana wa pekee wa Lambo na Shida. Alipendwa sana na watu. Lililowapendeza zaidi ni tabia yake ya upole na uaminifu. Hakuwa mbishi na mzembe. Alitii wavyele wake na kuwapa heshima. Alisikiliza nasaha za wavyele wake bila dharau.
Katika masomo, alikuwa wembe. Wanafunzi na walimu walimpenda sana. Matokeo yake ya mtihani wa mwisho yalidhihirisha zaidi kuwa alikuwa na bidii. Alama zake nyingi ziliwafanya walimu na wazazi wake waone fahari sana. Wazazi wake waliishi maisha ya uchochole sana. Hawakuweza kumlipia karo katika shule ya upili. Bendera alikataa tamaa.
Wazee wa zamani hawakukosea waliponena wema hauozi. Mzee Ndururu alisikia habari za Bendera. Alisikitika alipoelezwa kwamba masomo yake yangekatizwa kwa ajili ya karo. Aliwasiliana na wazazi wake na akamfadhili. Mzee Ndururu aliwaambia wazazi wa Bendera eti ashawahi kumvusha barabara kuu. Kutokana na tendo hilo la uadilifu, Mzee huyo aliamua kurudisha mkono. Kwa kweli maadili mema humfikisha mtu mbali.
9. Sentensi iliyopigiwa mstari ni fani gani ya lugha.
"Katika masomo, alikuwa wembe."
- AIsitiari
- BTashbihi
- CTasfida
- DTanakali za sauti
Answer
A. Isitiari
Bendera analinganishwa moja kwa moja na wembe bila neno "kama": hiyo ni isitiari.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Maadili ya Bendera yalimfikisha mbali.Question 10
- Fungu moja la mishororo katika shairi huitwaQuestion 11
- Vina vya mwisho vya shairi hili niQuestion 12
- Shairi hili ni la aina gani?Question 13
- Ujumbe wa ubeti wa pili wa shairi unahusu?Question 14
- Neno 'mahuluki' limetumika katika ubeti wa tatu. Lina maana yaQuestion 15