CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 3
Mtu ambaye hafanyishi mwili wake kazi au mazoezi anaweza kuwa mnene au
From Kiswahili — Assessment 2025 (Set 7) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo
Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali 1 hadi 5.
Amagu: Je, ulimwona ndugu Baro?
Seje: Yapita majuma mawili sijamwona.
Amagu: Siku hizi amenenepa na ana tumbo kubwa, sijui yeye hula nini?
Seje: Huenda ikawa hafanyi mazoezi ya mwili. Hukumbuki siku hizi hata uwanjani hapatikani. Nyumbani kwao kuna wafanyikazi wa kila kitu. Hata mezani haondoi sahani wala kupanguza.
Amagu: Maajabu hayo! Hata baada ya shibe ni kunyoosha miguu tu. Nakumbuka tukisoma hapo awali mwalimu Kisa alisema ukila chakula na usifanye kazi wala mazoezi unanenepa. Pia unaweza kupata magonjwa.
Seje: Kinyume ni kuwa dadake Amina ni mwembamba.
Amagu: Mimi humwona shambani kila siku. Ana bidii ya mchwa. Yeye hawezi kuwa hivyo.
Seje: Haya basi hebu tuelekee uwanjani. Leo nadhani tutazunguka uwanja mara kumi. Wengine wakifika tutacheza kandanda. Afya yetu ni muhimu.
3. Mtu ambaye hafanyishi mwili wake kazi au mazoezi anaweza kuwa mnene au
- AMwembamba
- BKutoonekana
- CMgonjwa
- DMchwa
Answer
C. Mgonjwa
Mwalimu Kisa alisema pia unaweza kupata magonjwa.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Tunaweza kulinda afya yetu kwa kula vizuri na kufanya nini?Question 4
- Siku hiyo vijana hawa waliimarisha afya yao kupitia mchezo gani?Question 5
- Bendera alikuwa na ndugu wangapi?Question 6
- Watu walimpenda Bendera kwa sababu hakuwaQuestion 7
- Wazazi wa Bendera walikuwaQuestion 8
- Sentensi iliyopigiwa mstari ni fani gani ya lugha. "Katika masomo, alikuwa wembe."Question 9