naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 2

Nani alielimisha vijana hawa jinsi ya kutunza mwili?

From Kiswahili — Assessment 2025 (Set 7) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo

Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali 1 hadi 5.
Amagu: Je, ulimwona ndugu Baro?
Seje: Yapita majuma mawili sijamwona.
Amagu: Siku hizi amenenepa na ana tumbo kubwa, sijui yeye hula nini?
Seje: Huenda ikawa hafanyi mazoezi ya mwili. Hukumbuki siku hizi hata uwanjani hapatikani. Nyumbani kwao kuna wafanyikazi wa kila kitu. Hata mezani haondoi sahani wala kupanguza.
Amagu: Maajabu hayo! Hata baada ya shibe ni kunyoosha miguu tu. Nakumbuka tukisoma hapo awali mwalimu Kisa alisema ukila chakula na usifanye kazi wala mazoezi unanenepa. Pia unaweza kupata magonjwa.
Seje: Kinyume ni kuwa dadake Amina ni mwembamba.
Amagu: Mimi humwona shambani kila siku. Ana bidii ya mchwa. Yeye hawezi kuwa hivyo.
Seje: Haya basi hebu tuelekee uwanjani. Leo nadhani tutazunguka uwanja mara kumi. Wengine wakifika tutacheza kandanda. Afya yetu ni muhimu.

2. Nani alielimisha vijana hawa jinsi ya kutunza mwili?

  1. AWazazi wao
  2. BDada Amina
  3. CNdugu Baro
  4. DMwalimu Kisa

Answer

D. Mwalimu Kisa

Amagu anakumbuka mwalimu Kisa alivyowafundisha.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test