CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 1
Mazungumzo yanahusu nini?
From Kiswahili — Assessment 2025 (Set 7) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo
Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali 1 hadi 5.
Amagu: Je, ulimwona ndugu Baro?
Seje: Yapita majuma mawili sijamwona.
Amagu: Siku hizi amenenepa na ana tumbo kubwa, sijui yeye hula nini?
Seje: Huenda ikawa hafanyi mazoezi ya mwili. Hukumbuki siku hizi hata uwanjani hapatikani. Nyumbani kwao kuna wafanyikazi wa kila kitu. Hata mezani haondoi sahani wala kupanguza.
Amagu: Maajabu hayo! Hata baada ya shibe ni kunyoosha miguu tu. Nakumbuka tukisoma hapo awali mwalimu Kisa alisema ukila chakula na usifanye kazi wala mazoezi unanenepa. Pia unaweza kupata magonjwa.
Seje: Kinyume ni kuwa dadake Amina ni mwembamba.
Amagu: Mimi humwona shambani kila siku. Ana bidii ya mchwa. Yeye hawezi kuwa hivyo.
Seje: Haya basi hebu tuelekee uwanjani. Leo nadhani tutazunguka uwanja mara kumi. Wengine wakifika tutacheza kandanda. Afya yetu ni muhimu.
1. Mazungumzo yanahusu nini?
- AMichezo
- BMaumbile
- CFamilia
- DAfya yetu
Answer
D. Afya yetu
Wanazungumza kuhusu kunenepa, mazoezi na magonjwa; Seje anamalizia, "Afya yetu ni muhimu."
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Nani alielimisha vijana hawa jinsi ya kutunza mwili?Question 2
- Mtu ambaye hafanyishi mwili wake kazi au mazoezi anaweza kuwa mnene auQuestion 3
- Tunaweza kulinda afya yetu kwa kula vizuri na kufanya nini?Question 4
- Siku hiyo vijana hawa waliimarisha afya yao kupitia mchezo gani?Question 5
- Bendera alikuwa na ndugu wangapi?Question 6
- Watu walimpenda Bendera kwa sababu hakuwaQuestion 7