naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 9

Omondi alifunga mabao mangapi?

From Kiswahili — End Term Assessment 2025 (Set 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma ufahamu kisha ujibu swali la 6 - 10.
Omondi ambaye alikuwa nyumbani akichunga kondoo na mbuzi sasa yuko shuleni. Ameingia kwa mara ya kwanza na amesoma mambo mengi sana mageni. Kila asubuhi badala ya kuelekea malishoni, kazi yake ni kuamka mapema kunawa, kustaftahi na kuwaaga wavyele wake. Tabia na mazoea yake bila shaka yamebadilika.
Huwa anapitia vichakani ambapo ni maskani ya simba na wanyama wengine hatari kama Nyati, Nyamaume na Nyoka. Bila shaka Simba ni hatari zaidi. Shuleni ni mbali na kitongoji chao anamoishi na inamlazimu kutembea kwa muda wa saa nzima. Baada ya masomo anaporudi nyumbani hupenda sana kumweleza mzazi wake mambo yote aliyosoma na kujifunza shuleni na sifa alizopata kwa kazi yake.
Siku moja alipata alama nyingi kwani alipata hesabu zote huko shuleni. Ilitokea kuwa siku hiyo kulikuwa na mchezo wa kandanda baada ya masomo saa kumi. Omondi kwa kuwa ni hodari katika mpira ilimlazimu akaucheze. Siku zote alikuwa mshambulizi matata. Siku hiyo alipata nafasi hiyo na kwa dakika chache akapachika bao la tatu wavuni. Bao hilo lilileta ushindi kwa timu yake. Mchezo ulikolea sana na watazamaji walizidi kumshangilia, "Omondi! Omondi! piga chenga! Heko!"

9. Omondi alifunga mabao mangapi?

  1. AMatatu
  2. BMoja
  3. CMengi
  4. DHatujaelezwa.

Answer

D. Hatujaelezwa.

Kifungu kinasema alifunga bao la tatu la timu, lakini hakisemi alifunga mabao mangapi yeye mwenyewe.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test