naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 3

Mamake Kadoti alishtakiwa kwa kosa gani?

From Kiswahili — End Term 1 Exam 2025 (Set 3) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma hadithi hii kisha ujibu maswali.
Kadoti alikuwa anasafiri pamoja na familia yake. Walikuwa wanatembea mbuga ya wanyama ya Nakuru. Walikuwa wamebeba chakula na matunda. Kadoti alikuwa ameketi katika kiti cha nyuma ya gari lao. Mara alipohisi njaa, alichukua nyama ya kuku na kuila. Mifupa alitupa nje kupitia kwenye dirisha la gari. Alikuwa anateremsha kioo kisha anatupa uchafu nje. Mamake alimwonya dhidi ya kufanya hivyo. Alimwambia kuwa uchafuzi wa mazingira haukubaliwi na sheria za nchi. Walipokuwa wanapita mji wa Nakuru, Kadoti alitoa ndizi mbili. Akatoa maganda akala, kisha akatupa hayo maganda nje. Baada ya mita chache gari lao lilisimamishwa na askari wa baraza la mji. Mamake Kadoti alishtakiwa kwa kuruhusu mtoto kutupa taka katika barabara za mji. Alijitetea lakini askari hakumsikiliza. Alitozwa faini. Hapo ndipo Kadoti alijifunza kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.

3. Mamake Kadoti alishtakiwa kwa kosa gani?

Answer

Kumruhusu mtoto kutupa taka barabarani

"alishtakiwa kwa kuruhusu mtoto kutupa taka katika barabara za mji."

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test