CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term Exam 2025 · Question 4
Inaonekana Maria na Rukia ni
From Kiswahili — Midterm Assessment 2025 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma mazungumzo haya kwa makini kisha ujibu maswali yanayofuata.
(Maria na Rukia wanakutana. Mazungumzo yao yanakuwa hivi)
Maria: Masalheri Rukia.
Rukia: Aheri Maria. Naona umeniwahi kufika leo.
Maria: (Akitabasamu) Nimefika muda mfupi tu uliopita yapata nusu saa hivi.
Rukia: Nusu saa! Huo si muda mfupi. Lazima umefaidi maonyesho mengi kabla sijafika.
Maria: Kipendacho moyo ni dawa. Ninayapenda maonyesho ya kitamaduni kwani hunipa fursa ya kipekee ya kujifunza tamaduni za wengine.
Rukia: Hayo ni ya kweli ndugu yangu. Isitoshe, tukifurahia tamaduni za wenzetu, tutaelewa zaidi. Hii ni njia muhimu ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
Maria: Naam, hali kadhalika, uigizaji ni njia mojawapo ya kutambua na kukuza vipawa vyetu.
Rukia: (Akiwatazama vijana walio jukwaani) Hilo linanikumbusha kwamba tulilipa kiingilio ili tupate nafasi hapa ukumbini. Haikosi waigizaji hawa watapata ujira wao kutokana na malipo hayo. Kwa hivyo tamasha hizi kwa wengine ni njia ya kupata riziki.
Maria: Maigizo yenyewe huwa na malengo ya kuonya dhidi ya maovu katika jamii, kuelimisha na kupinga mila mbovu.
Rukia: Naona jukwaa li tayari sasa. (Anatua kidogo) Ni heri tutulie ili tusipitwe na uhondo.
Maria: Sawa dada yangu. (Wanatulia kutazama mchezo jukwaani).
4. Inaonekana Maria na Rukia ni
- Andugu
- Bmaadui
- Cwaigizaji
- Dwazee.
Answer
A. ndugu
Wanaitana "ndugu yangu" na "dada yangu".
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Maria na Rukia walienda kutazama maonyesho wapi?Question 5
- Ufahamu huu unazungumzia nini?Question 6
- Ipi kati ya hizi si njia ambayo watu hushiriki ufisadi kulingana na kifungu?Question 7
- Kulingana na kifungu hiki, ufisadi husababisha nini?Question 8
- Ni jukumu la nani kukomesha ufisadi?Question 9
- Ni methali ipi inaweza kutumika kueleza ujumbe katika aya ya mwisho?Question 10