CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 5
Katika mazungumzo, neno "mazingira" linamaanisha nini?
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
(Mama ameketi sebuleni akitazama runinga. Anaizima televisheni anapomwona Tina akiingia.)
Tina: (Akimkaribia Mama) Shikamoo mama?
Mama: (Kwa furaha) Marahaba mwanangu karibu nyumbani. Habari za shule?
Tina: Njema mama! Leo nina furaha sana.
Mama: Haya basi, nipe habari. Furaha ni ya nini?
Tina: Leo nimepewa tuzo ya mchoraji maarufu. Nilishinda tuzo hii baada ya kushiriki shindano lililohusu elimu ya mazingira.
Mama: Hongera mwanangu! Kazi nzuri sana.
Tina: Mchoro wangu ulionyesha wanafunzi wakipiga deki na kudumisha usafi wa mazingira ya shule.
Mama: Aha! Kumbe wewe ni gwiji mwanangu. Haya basi, endelea kufanya mazoezi zaidi ili kuboresha talanta yako.
Tina: Asante mama. Mama, ninaweza kufanya nini tena ili kuwa bora zaidi katika sanaa ya uchoraji?
Mama: Kumbuka kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame, hivyo basi lazima ujitahidi sana ili uwe mchoraji hodari.
Tina: Ni kweli mama, nadhani ni muhimu pia kushirikiana na wachoraji wenzangu ili kukiboresha kipawa changu.
Mama: Naam, mwanangu. Aidha ni jambo zuri kushiriki mashindano ya mara kwa mara. Yatakuboresha zaidi.
5. Katika mazungumzo, neno "mazingira" linamaanisha nini?
- AHali au vitu vinavyomzunguka kiumbe.
- BShule anayosomea mwanafunzi.
- CMasomo yanayohusu viumbe hai.
- DUsafi wa eneo la shule pekee.
Answer
A. Hali au vitu vinavyomzunguka kiumbe.
Mazingira ni vitu vinavyotuzunguka.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Ni kitendo kipi kinachoonyesha kwamba Mwafrika aliwajali jirani zake?Question 6
- Kwa nini masuala ya mgeni yalipewa kipaumbele katika jamii nyingi za Kiafrika?Question 7
- Mgeni akiwa na tabia isiyopendeza, wenyeji walifanya nini?Question 8
- Kwa nini mgeni alichinjiwa mnyama siku ya kwanza alipowasili?Question 9
- Nyama, maharagwe na mayai ni vyakula vya aina gani?Question 10
- Kulingana na kifungu, ni haki ngapi za watoto zilizotajwa?Question 11