naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 3

Methali "Mtaka cha mvunguni sharti ainame" ina maana ya kujitahidi ili kufanikiwa. Ni methali ipi iliyo tofauti kimaana na hiyo?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
(Mama ameketi sebuleni akitazama runinga. Anaizima televisheni anapomwona Tina akiingia.)
Tina: (Akimkaribia Mama) Shikamoo mama?
Mama: (Kwa furaha) Marahaba mwanangu karibu nyumbani. Habari za shule?
Tina: Njema mama! Leo nina furaha sana.
Mama: Haya basi, nipe habari. Furaha ni ya nini?
Tina: Leo nimepewa tuzo ya mchoraji maarufu. Nilishinda tuzo hii baada ya kushiriki shindano lililohusu elimu ya mazingira.
Mama: Hongera mwanangu! Kazi nzuri sana.
Tina: Mchoro wangu ulionyesha wanafunzi wakipiga deki na kudumisha usafi wa mazingira ya shule.
Mama: Aha! Kumbe wewe ni gwiji mwanangu. Haya basi, endelea kufanya mazoezi zaidi ili kuboresha talanta yako.
Tina: Asante mama. Mama, ninaweza kufanya nini tena ili kuwa bora zaidi katika sanaa ya uchoraji?
Mama: Kumbuka kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame, hivyo basi lazima ujitahidi sana ili uwe mchoraji hodari.
Tina: Ni kweli mama, nadhani ni muhimu pia kushirikiana na wachoraji wenzangu ili kukiboresha kipawa changu.
Mama: Naam, mwanangu. Aidha ni jambo zuri kushiriki mashindano ya mara kwa mara. Yatakuboresha zaidi.

3. Methali "Mtaka cha mvunguni sharti ainame" ina maana ya kujitahidi ili kufanikiwa. Ni methali ipi iliyo tofauti kimaana na hiyo?

  1. AUmoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
  2. BAchanikaye kwenye mpini hafi njaa.
  3. CMgaagaa na upwa hali wali mkavu.
  4. DMchumia juani hulia kivulini.

Answer

A. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

Methali nyingine zote zinahusu bidii; A inahusu umoja.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test