naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 1

Tina alipoulizwa na mama yake kuhusu hali ya shule, alijibu vipi?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
(Mama ameketi sebuleni akitazama runinga. Anaizima televisheni anapomwona Tina akiingia.)
Tina: (Akimkaribia Mama) Shikamoo mama?
Mama: (Kwa furaha) Marahaba mwanangu karibu nyumbani. Habari za shule?
Tina: Njema mama! Leo nina furaha sana.
Mama: Haya basi, nipe habari. Furaha ni ya nini?
Tina: Leo nimepewa tuzo ya mchoraji maarufu. Nilishinda tuzo hii baada ya kushiriki shindano lililohusu elimu ya mazingira.
Mama: Hongera mwanangu! Kazi nzuri sana.
Tina: Mchoro wangu ulionyesha wanafunzi wakipiga deki na kudumisha usafi wa mazingira ya shule.
Mama: Aha! Kumbe wewe ni gwiji mwanangu. Haya basi, endelea kufanya mazoezi zaidi ili kuboresha talanta yako.
Tina: Asante mama. Mama, ninaweza kufanya nini tena ili kuwa bora zaidi katika sanaa ya uchoraji?
Mama: Kumbuka kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame, hivyo basi lazima ujitahidi sana ili uwe mchoraji hodari.
Tina: Ni kweli mama, nadhani ni muhimu pia kushirikiana na wachoraji wenzangu ili kukiboresha kipawa changu.
Mama: Naam, mwanangu. Aidha ni jambo zuri kushiriki mashindano ya mara kwa mara. Yatakuboresha zaidi.

1. Tina alipoulizwa na mama yake kuhusu hali ya shule, alijibu vipi?

  1. ANzuri
  2. BNjema
  3. CMarahaba
  4. DShikamoo

Answer

B. Njema

"Njema mama!"

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test