CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 7
Unafikiri ni nini kingetokea iwapo bodaboda ingeendeshwa taratibu?
From Kiswahili — School Based Assessment 2025 (Set 11B) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Ilikuwa siku ya soko katika kijii cha Rukano. Daima Sokwe hakukosa kufika sokoni kuuza maembe na maparachichi aliyoyakuza. Alikuwa mkulima hodari wa matunda hayo.
Baada ya kujiandaa, Sokwe aliyapanga matunda yake katika kapu. Aliitazama saa yake ya mkono. Ilikuwa saa moja na robo!
“Nitachelewesha wateja wangu!” Sokwe alijisemea.
Alishika njia kuelekea kwa rafiki yake Korongo ili aandamane naye. Korongo alikuwa mkulima wa mpunga. Punde tu alipofika kwenye barabara iliyokuwa mkabala na makazi ya Korongo, Sokwe alimwona akitembea kwa kasi. Alilibeba kapu lake la mchele mgongoni huku akihema. “Hata wewe uliamka ukiwa umechelewa?” Sokwe alimuuliza.
“Aka! Sikutaraji hata kuamka leo rafiki yangu. Nahisi maumivu mwilini. Hii kazi ya kijungu jiko! ” Alijibu Korongo.
Korongo alilalamikia uzito wa mzigo aliokuwa nao. Alipendekeza watumie bodaboda. Sokwe alikubaliana naye. Basi wakaabiri bodaboda iliyokuwa inaendeshwa na Mbuni. Walizidi kumrai Mbuni aongeze kasi. Walitaka kufika sokoni haraka. Hawakukumbuka, haraka haraka haina baraka!
Mbuni alishindwa kuidhibiti bodaboda ile kwenye mteremko. Ilianguka. Makapu yalianguka ovyo! Matunda yalizagaa barabarani. Sokwe na Korongo waliumia. Hawakuwa wamevaa helmeti. Hawakutahadhari kabla ya hatari. Njiwa na Mwewe waliokuwa karibu waliwaokoa na kuwapeleka hospitalini. Safari ilikuwa imetumbukia nyongo.
7. Unafikiri ni nini kingetokea iwapo bodaboda ingeendeshwa taratibu?
Answer
Hawangepata ajali
Haraka haraka haina baraka.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Safari ilikuwa imetumbukia nyongo ina maana:Question 8
- Msimulizi alijifunza upishi kutoka kwa nani?Question 9
- Mama alimpa msimulizi jina ‘mpishi bora’. Eleza sababu.Question 10
- Ni nini kingefanyika iwapo msimulizi angekosa kupika chakula kitamu?Question 11
- Methali, chanda chema huvikwa pete katika kifungu inaeleza nini kuhusu msimulizi?Question 12
- Je, Zubeda alienda katika ofisi ya mwalimu wakati gani?Question 13