naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 6

Ni mambo gani yanayoonyesha kuwa Sokwe na Korongo walitaka kufika sokoni mapema?

From Kiswahili — School Based Assessment 2025 (Set 11B) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Ilikuwa siku ya soko katika kijii cha Rukano. Daima Sokwe hakukosa kufika sokoni kuuza maembe na maparachichi aliyoyakuza. Alikuwa mkulima hodari wa matunda hayo.
Baada ya kujiandaa, Sokwe aliyapanga matunda yake katika kapu. Aliitazama saa yake ya mkono. Ilikuwa saa moja na robo!
“Nitachelewesha wateja wangu!” Sokwe alijisemea.
Alishika njia kuelekea kwa rafiki yake Korongo ili aandamane naye. Korongo alikuwa mkulima wa mpunga. Punde tu alipofika kwenye barabara iliyokuwa mkabala na makazi ya Korongo, Sokwe alimwona akitembea kwa kasi. Alilibeba kapu lake la mchele mgongoni huku akihema. “Hata wewe uliamka ukiwa umechelewa?” Sokwe alimuuliza.
“Aka! Sikutaraji hata kuamka leo rafiki yangu. Nahisi maumivu mwilini. Hii kazi ya kijungu jiko! ” Alijibu Korongo.
Korongo alilalamikia uzito wa mzigo aliokuwa nao. Alipendekeza watumie bodaboda. Sokwe alikubaliana naye. Basi wakaabiri bodaboda iliyokuwa inaendeshwa na Mbuni. Walizidi kumrai Mbuni aongeze kasi. Walitaka kufika sokoni haraka. Hawakukumbuka, haraka haraka haina baraka!
Mbuni alishindwa kuidhibiti bodaboda ile kwenye mteremko. Ilianguka. Makapu yalianguka ovyo! Matunda yalizagaa barabarani. Sokwe na Korongo waliumia. Hawakuwa wamevaa helmeti. Hawakutahadhari kabla ya hatari. Njiwa na Mwewe waliokuwa karibu waliwaokoa na kuwapeleka hospitalini. Safari ilikuwa imetumbukia nyongo.

6. Ni mambo gani yanayoonyesha kuwa Sokwe na Korongo walitaka kufika sokoni mapema?

Answer

Waliamua kuabiri bodaboda; walizidi kumrai Mbuni aongeze kasi

Walitaka kufika haraka.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test