naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 4

Eleza maana ya “kutuliza hali” kulingana na kifungu.

From Kiswahili — School Based Assessment 2025 (Set 11B) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Mashindano ya soka baina ya shule za msingi yamekaribia. Kocha wa timu ya shule ya msingi ya Kinja ni mwingi wa hofu kwa sababu huenda mchezaji hodari wa kikosi chake, Kiki Malala asishiriki. Kiungo huyo wa safu ya kati, alijeruhiwa majuma mawili yaliyopita kwenye mechi ya kujipima nguvu baina ya timu ya Kinja na wenyeji, Mtwana.
Mechi hiyo iliyosakatiwa katika uwanja wa shule ya Mtwana ilisitishwa katika dakika ya sitini baada ya mtafaruku kuanza. Mashabiki wa timu ya Mtwana walianza kuzunguka uwanjani wakiimba nyimbo za kukejeli timu pinzani. Nyimbo hizo ziliwakasirisha mashabiki wa timu ya Kinja ambao walisababisha rabsha. Mashabiki waliingia uwanjani na kuwafanya wachezaji kukimbilia usalama wao. Ni wakati huo ambapo mchezaji, Kiki Malala alijikwaa na kuteguka mguu.
Hali hii ilidhibitiwa baada ya muda mfupi. Vikosi vya maskauti vilishirikiana kutuliza hali. Hata hivyo, mechi haikuweza kuendelea. Akihutubia wanahabari baada ya mechi hiyo, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Mtwana alikashifu vikali kitendo hicho. Alisema, “Mashindano ya mpira si uadui. Hayafai kututenganisha. Ni sharti kila shabiki ashangilie timu yake kwa amani.” Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kinja ambaye alisema daima shule zao zitabaki kuwa marafiki. Kadhalika aliwasuta wachochezi kwa kujaribu kuvuruga mchuano wa kirafiki. Aliwataka mashabiki na wachezaji daima kukubali matokeo ya mpira, kwani asiyekubali kushindwa si mshindani.

4. Eleza maana ya “kutuliza hali” kulingana na kifungu.

Answer

Kurejesha utulivu

Kumaliza mtafaruku.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test