CBC Grade 5 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 36
b) Watu walitaka kumwona nani akifunga ndoa?
From Kiswahili — End Term 2 Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.
Ilikuwa likizo ya mwezi wa Aprili. Mimi na dada yangu Pendo tulihudhuria harusi ya shangazi yetu aitwaye Zainabu. Tulialikwa kubeba pete za bibi na bwana harusi. Watu wengi walihudhuria harusi hiyo iliyokuwa ya kufana sana. Kila mtu alifurahia kuona shangazi yetu akifunga ndoa na mpenzi wake Jabali.
Kulikuwa na vyakula vingi kama keki na vinywaji vya aina mbalimbali. Baada ya sherehe, shangazi yetu na mume wake walipanda ndege na kusafiri kwenda Uarabuni.
11. b) Watu walitaka kumwona nani akifunga ndoa?
Answer
Shangazi yao Zainabu
Kila mtu alifurahia kumwona shangazi.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.