CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 1
Tito na Meta walikutana wapi? (1 alama)
From Kiswahili — Midterm Term 2 Assessment 2026 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1–8.
Tito: (Akiwa hotelini, anaonyesha njaa) Aah bwana Meta, njaa imenibana sana. Ni saa ngapi?
Meta: Saa nne kasorobo asubuhi.
Tito: Lo! Ni mapema sana. Njaa haina saa jameni bwana Meta.
Meta: Je, hukunywa chai kwa mama mkubwa?
Tito: La! (akitikisa kichwa) sikunywa. Mjomba Karama aliniamsha alfajiri na kunituma kwa binti Mawazo.
Meta: Kufanya nini, ndugu Tito?
Tito: Kumpasha ujumbe kuhusu harusi ya mama Zedi itakayofanyika Jumamosi saa tatu asubuhi.
Meta: Aha! Niliona ukumbi wa sherehe ukiandaliwa jana. Kumbe hayo ni maandalizi ya harusi hiyo.
Tito: Naam. Bibi Mwendo ndiye anayesimamia mipango yote ya harusi. Ana ujuzi mkubwa wa mambo hayo.
Meta: Kweli. Haya basi, tutawaagiza watuandalia chai ya saa nne.
Tito: Naam. Hakika napenda vyakula vya kiasili. Nitashukuru kupata chai na viazi vitamu.
1. Tito na Meta walikutana wapi? (1 alama)
Answer
Hotelini
Mwanzoni: "Akiwa hotelini".
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Ni nini kilichomshangaza Meta? (1 alama)Question 2
- Kwa nini Tito hakuwa amekunywa chai asubuhi? (1 alama)Question 3
- Tito alikuwa amepeleka ujumbe wa nini? (1 alama)Question 4
- Ni nani aliyesimamia maandalizi ya sherehe? (1 alama)Question 5
- Ni nani alikuwa akisherehekea harusi? (1 alama)Question 6
- Ni chakula gani Tito alitarajia kupewa? (1 alama)Question 7