naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 3

Kwa nini Tito hakuwa amekunywa chai asubuhi? (1 alama)

From Kiswahili — Midterm Term 2 Assessment 2026 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1–8.
Tito: (Akiwa hotelini, anaonyesha njaa) Aah bwana Meta, njaa imenibana sana. Ni saa ngapi?
Meta: Saa nne kasorobo asubuhi.
Tito: Lo! Ni mapema sana. Njaa haina saa jameni bwana Meta.
Meta: Je, hukunywa chai kwa mama mkubwa?
Tito: La! (akitikisa kichwa) sikunywa. Mjomba Karama aliniamsha alfajiri na kunituma kwa binti Mawazo.
Meta: Kufanya nini, ndugu Tito?
Tito: Kumpasha ujumbe kuhusu harusi ya mama Zedi itakayofanyika Jumamosi saa tatu asubuhi.
Meta: Aha! Niliona ukumbi wa sherehe ukiandaliwa jana. Kumbe hayo ni maandalizi ya harusi hiyo.
Tito: Naam. Bibi Mwendo ndiye anayesimamia mipango yote ya harusi. Ana ujuzi mkubwa wa mambo hayo.
Meta: Kweli. Haya basi, tutawaagiza watuandalia chai ya saa nne.
Tito: Naam. Hakika napenda vyakula vya kiasili. Nitashukuru kupata chai na viazi vitamu.

3. Kwa nini Tito hakuwa amekunywa chai asubuhi? (1 alama)

Answer

Aliamshwa alfajiri na kutumwa kwa binti Mawazo.

Mjomba Karama alimtuma.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test