CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 7
Ni chakula gani Tito alitarajia kupewa? (1 alama)
From Kiswahili — Midterm Term 2 Assessment 2026 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1–8.
Tito: (Akiwa hotelini, anaonyesha njaa) Aah bwana Meta, njaa imenibana sana. Ni saa ngapi?
Meta: Saa nne kasorobo asubuhi.
Tito: Lo! Ni mapema sana. Njaa haina saa jameni bwana Meta.
Meta: Je, hukunywa chai kwa mama mkubwa?
Tito: La! (akitikisa kichwa) sikunywa. Mjomba Karama aliniamsha alfajiri na kunituma kwa binti Mawazo.
Meta: Kufanya nini, ndugu Tito?
Tito: Kumpasha ujumbe kuhusu harusi ya mama Zedi itakayofanyika Jumamosi saa tatu asubuhi.
Meta: Aha! Niliona ukumbi wa sherehe ukiandaliwa jana. Kumbe hayo ni maandalizi ya harusi hiyo.
Tito: Naam. Bibi Mwendo ndiye anayesimamia mipango yote ya harusi. Ana ujuzi mkubwa wa mambo hayo.
Meta: Kweli. Haya basi, tutawaagiza watuandalia chai ya saa nne.
Tito: Naam. Hakika napenda vyakula vya kiasili. Nitashukuru kupata chai na viazi vitamu.
7. Ni chakula gani Tito alitarajia kupewa? (1 alama)
Answer
Chai na viazi vitamu
Sentensi ya mwisho.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Eleza hali ya Tito mwanzoni mwa mazungumzo. (2 alama)Question 8
- Chumba maalum cha kupokelea wageni huitwa nini? (1 alama)Question 16
- Andika neno ambalo si nomino ya wingi. (1 alama)Question 17
- Andika neno la heshima linalotumika kumshukuru mtu. (1 alama)Question 18
- Kamilisha sentensi: Uwanja ___ unapendeza. (1 alama)Question 19
- Andika kinyume cha neno mfupi. (1 alama)Question 20