CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 6
Neno alfajiri limetumiwa kumaanisha nini?
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6–10.
Mtu huamka alfajiri ili kuanza shughuli za siku mpya. Mja anayeamka mapema huweza kupanga mambo yake kulingana na saa. Pia huweza kutekeleza wajibu wake ipasavyo bila wasiwasi. Shughuli hizi ndizo hujenga taifa.
Baadhi ya kazi zinazojenga taifa letu ni kama vile ualimu, ukarani, udereva, ukulima na biashara. Kuna wafanyakazi wanaoingia kazini macheo na kutoka machweo. Wakati wa adhuhuri kila mmoja hutafuta chamcha. Baadhi yao hula sima, wali, nyama ya kuku, sukuma wiki na maharagwe. Kuna wafanyakazi wanaopenda kunywa chai wakati wa alasiri kisha kuelekea nyumbani jioni.
6. Neno alfajiri limetumiwa kumaanisha nini?
- AUsiku wa manane
- BUsiku
- CJioni
- DAsubuhi mapema
Answer
D. Asubuhi mapema
Alfajiri ni asubuhi mapema kabla ya jua kuchomoza.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Kati ya maneno haya, lipi linaweza kutumiwa badala ya neno mja?Question 7
- Kazi ipi haijatajwa kama inayojenga taifa?Question 8
- Chakula kinacholiwa wakati wa adhuhuri huitwa nini?Question 9
- Wakati wa machweo ni upi?Question 10
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 11.Question 11
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 12.Question 12