naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Mock Exam 2025 · Question 9

Sungura alimwambia Simba akale wanyama gani?

From Kiswahili — First Trial Assessment 2025 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma ufahamu kisha jibu swali la 6 - 10.
Hapo zamani kulikuwa na Simba aliyejulikana kama mfalme wa wanyama wote porini. Siku moja aliamua kumtembelea Sungura aliyejulikana kuwa mwerevu na mjanja sana kule porini. Basi, Simba alipofika nyumbani kwa Sungura mjanja, Sungura akatoka akamkaribisha akae. Simba akakataa kukaa akamwambia, 'Mimi nina njaa kweli, sijala siku ya tatu sasa. Swara na Nyumbu ambao ndio chakula chetu ukoo wa kifalme wamegoma, wanasema tusubiri hadi mmoja wao afe ndio tule mzoga.' Akaendelea kumwambia Sungura, 'Mgomo huu umetushangaza sana familia ya kifalme na katika kikao chetu cha ikulu jana tumeamua kuwa kwa sababu nyinyi ni majirani na ni wengi, basi nyinyi ndio mtakuwa chakula chetu.' Sungura wakati huo alikuwa anamsikiliza kwa makini sana. Baada ya maelezo marefu kutoka kwa Simba kuhusu maamuzi ya familia ya kifalme, Sungura akamwambia, 'Lakini mfalme, kwa nini uhangaike kutafuta chakula wakati mnazaa vitoto vingi hivyo? Sisi Sungura tuko wadogo kama vile vitoto vyenu na hata nyama ya vitoto vyenu ni tamu kuliko yetu.' Simba baada ya kusikiliza kwa makini akamshukuru Sungura kwa ushauri wake akarudi nyumbani. Alipofika tu nyumbani akaanza kukamata vitoto vyake na kuvila. Alipokuja mama wa vitoto vile akakuta vitano vimeshaliwa tayari. Simba jike akaanza kugombana na kupigana na mumewe.
Baada ya ugomvi Simba jike akamuuliza dume, 'Kwa nini umefanya kitendo kibaya namna hii?' Simba dume akajibu, 'Ni shauri ya Sungura, kaniambia watoto wetu ni watamu kuliko wao.'
Simba jike alikasirika sana akamwendea Sungura mbio. Sungura kuona hivyo akatoka na mkuki. Wakaanza kufukuzana hadi kwenye kichuguu, Sungura akaingia kwenye shimo. Simba akakamata mkia akaanza kuvuta. Sungura alipoona kashikwa mkia akamwambia Simba, 'Mbona unaacha kushika mkia unashika mzizi wa mti?' Simba kusikia hivyo akaachia mkia wa Sungura akashika mzizi wa mti akidhani ndio mkia wa Sungura. Sungura akamwambia, 'Shikilia hapo, vuta kwa nguvu.' Sungura akajichimbia chini zaidi na Simba hakuambulia kitu, akarudi nyumbani kwa huzuni.

9. Sungura alimwambia Simba akale wanyama gani?

  1. AWadogo.
  2. BWale wamelala.
  3. CWatoto wake.
  4. DWazee ambao wako karibu kufa.

Answer

C. Watoto wake.

Sungura alisema nyama ya vitoto vya Simba ni tamu kuliko yao.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test