CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 7
Ni sehemu gani ya mwili wa ndege inayomsaidia kupata joto?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 7 – 10.
Ndege wa porini ni viumbe wa kuvutia wanaoishi katika mazingira asili kama vile misitu, nyika na porini. Ndege hawa hawategemei msaada wa binadamu. Mifano ya ndege hao ni chiriku, tai, mbuni, kanga, mwewe na heroe. Wana uwezo wa kujenga viota juu ya miti au kwenye nyasi ndefu ili kulinda mayai na vifaranga wao. Miili yao imefunikwa kwa manyoya yanayowapa joto. Wana mabawa yenye nguvu ya kupaa angani, kutafuta chakula au kutoroka maadui.
Pia, wana vidona vya kuokota mbegu, wadudu au kuwinda wanyama wadogo. Kwa mfano, mbuni ni ndege mkubwa asiyepaa na ana uwezo wa kukimbia kwa kasi ya ajabu akitumia miguu yake. Ni jukumu letu kulinda mazingira ya ndege hawa kwa kutoharibu misitu na vyanzo vya maji ili vizazi vyao viendelee, kufurahia nyimbo zao tamu.
7. Ni sehemu gani ya mwili wa ndege inayomsaidia kupata joto?
- AKiota
- BVidona
- CManyoya
- Dmabawa
Answer
C. Manyoya
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Kwa nini ndege hujenga viota juu ya miti au nyasi ndefu?Question 8
- Taja sifa moja ya mbuni ilivyoelezwa katika ufahamu.Question 9
- Kichwa kinachofaa ufahamu huu ni kipi?Question 10
- Ni kipi hakikutumika kutengeneza mapambo ya asili.Question 11
- Kulingana na ufahamu, ni mambo gani yametajwa kuwa pambo kuu la kudumu?Question 12
- Chagua mapambo ya kisasa peke yake.Question 13