CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 9
Taja sifa moja ya mbuni ilivyoelezwa katika ufahamu.
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 7 – 10.
Ndege wa porini ni viumbe wa kuvutia wanaoishi katika mazingira asili kama vile misitu, nyika na porini. Ndege hawa hawategemei msaada wa binadamu. Mifano ya ndege hao ni chiriku, tai, mbuni, kanga, mwewe na heroe. Wana uwezo wa kujenga viota juu ya miti au kwenye nyasi ndefu ili kulinda mayai na vifaranga wao. Miili yao imefunikwa kwa manyoya yanayowapa joto. Wana mabawa yenye nguvu ya kupaa angani, kutafuta chakula au kutoroka maadui.
Pia, wana vidona vya kuokota mbegu, wadudu au kuwinda wanyama wadogo. Kwa mfano, mbuni ni ndege mkubwa asiyepaa na ana uwezo wa kukimbia kwa kasi ya ajabu akitumia miguu yake. Ni jukumu letu kulinda mazingira ya ndege hawa kwa kutoharibu misitu na vyanzo vya maji ili vizazi vyao viendelee, kufurahia nyimbo zao tamu.
9. Taja sifa moja ya mbuni ilivyoelezwa katika ufahamu.
- ANi ndege anayepaa angani
- BKukimbia kwa kasi ajabu akitumia miguu
- CKuwinda wanyama wadogo
- DKutoroka maadui
Answer
B. Kukimbia kwa kasi ajabu akitumia miguu
Hukimbia kwa kasi.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Kichwa kinachofaa ufahamu huu ni kipi?Question 10
- Ni kipi hakikutumika kutengeneza mapambo ya asili.Question 11
- Kulingana na ufahamu, ni mambo gani yametajwa kuwa pambo kuu la kudumu?Question 12
- Chagua mapambo ya kisasa peke yake.Question 13
- Ni nini maana ya msemo “kukata tamaa”?Question 14
- Kwa jumla, ufahamu huu unazungumzia nini?Question 15