naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2025 · Question 20

Kulingana na habari, ni kweli kusema kuwa

From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2025 (Set 10) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1 hadi 3.

Dukakuu la Tulizo liko katika kaunti ya Konambaya. Ingawa kunayo madukakuu mengine, Tulizo ndilo kubwa zaidi. Limejengwa kando ya barabara kuu ya Jogoo katikati ya kituo cha polisi cha Pingu na soko la Malimali. Mwenye duka hilo anaitwa bwana Sahara. Bwana Sahara amewaajiri wafanyakazi sita. Wengi wao ni wanaume. Hata hivyo, wanawake wachache waliomo hufanya kazi nyepesi nyepesi tu. Bwana Sahara huhakikisha kuwa wateja wote wamehudumiwa vyema. Huwataka waende wakiwa wameridhika. Wakazi wengi hulipenda duka hili la bwana Sahara kwa sababu humo, wao hupata kila wanachohitaji kutoka unga hadi matunda.

1. Kulingana na habari, ni kweli kusema kuwa

  1. Akunayo maduka mengine makubwa Konambaya.
  2. Bbarabara ya Jogoo iko kati ya soko na kituo cha polisi.
  3. Cbwana Sahara hawezi kufanya kazi peke yake dukani mle.
  4. Dkuna bidhaa chache dukani Tulizo.

Answer

C. bwana Sahara hawezi kufanya kazi peke yake dukani mle.

Bwana Sahara ameajiri wafanyakazi sita, kwa hivyo hawezi kufanya kazi peke yake. Tulizo ndilo duka kubwa zaidi, na lina kila kitu.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test