naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 5

Basi linalotoka Dinda kuelekea mjini linaitwaje?

From Kiswahili — CBC Assessment 2025 Set 1 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu swali la 6 - 10.

Sisi tunaishi katika kijiji cha Dinda. Hapa kijijini basi huondoka na kurudi kila siku. Basi hilo linaitwa Manyanga. Manyanga huanza safari yake kila siku alfajiri. Likikaribia kituoni hupiga honi kwa nguvu. Wasafiri hulisubiri basi kituoni. Wale wanaochelewa hukimbia ili kuliwahi.

Watu hukaa kwenye viti mapema, kisha basi huondoka kuelekea mjini. Basi linapofika mjini, watu wote hushuka na kuingia katika shughuli zao. Dereva hupeleka basi kwenye kituo cha mafuta na kulijaza mafuta. Baada ya kujaza mafuta, yeye hulirudisha kituoni. Watu wanaokwenda kijijini huanza kupanda kwenye basi. Kondakta huingia na hupokea nauli huku akitoa tiketi.

Ikifika saa nane, Manyanga huanza safari ya kurudi kijijini. Basi hilo hubeba mizigo mingi ya madukani na mingine ya abiria. Linapofika karibu na kituo cha kwetu, hupiga honi. Watu wengi huenda barabarani kupokea wageni wao. Wengine huenda kupokea mizigo yao iliyoletwa na basi hilo. Tukifunga shule, mimi na dada yangu tutasafiri kwa Manyanga kwenda mjini kumsalimia kaka.

6. Basi linalotoka Dinda kuelekea mjini linaitwaje?

  1. AManyanga
  2. BBasi kuu
  3. CBebabeba
  4. DMatwana.

Answer

A. Manyanga

Hadithi inasema: "Basi hilo linaitwa Manyanga."

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test