CBC Grade 4 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 4
Baba yake Pendo alimwambia kuwa angemtumia shilingi ngapi?
From Kiswahili — CBC Assessment 2025 Set 1 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 1 hadi 5.
(Pendo akiwa kwenye simu akiongea na baba yake)
Baba: Halo Pendo.
Pendo: Halo baba, shikamoo.
Baba: Marahaba mwanangu, hujambo?
Pendo: Sijambo baba. Vipi nyie huko?
Baba: Hata sisi tu wazima. Mama na ndugu zako wanaendelea vizuri. Unaendeleaje na masomo?
Pendo: Naendelea vyema. Walimu wetu ni wazuri. Tunafurahia sana masomo.
Baba: Zingatia sana masomo mwanangu. Je una mahitaji yoyote?
Pendo: Nahitaji pesa za kununulia mahitaji binafsi.
Baba: Sawa nitatuma shilingi elfu tano. Mwalimu Paulo atakutunzia. Atakuwa anakupa unapohitaji.
Pendo: Asante baba.
Baba: Haya, nakutakia masomo mema mwanangu.
Pendo: Asante, wasalimie wadogo zangu.
5. Baba yake Pendo alimwambia kuwa angemtumia shilingi ngapi?
- A500
- B5000
- C50000
- D500000
Answer
B. 5000
Baba anasema atatuma "shilingi elfu tano". Elfu tano ni 5000.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Basi linalotoka Dinda kuelekea mjini linaitwaje?Question 5
- Basi hili huanza safari yake wakati gani?Question 6
- Manyanga likikaribia kituoni hufanya nini?Question 7
- Mwendo wa saa nane, Manyanga huanza safari kuelekea wapi?Question 8
- Anayepokea nauli na kupeana tiketi ni nani?Question 9
- Marafiki hawa walikuwa akina nani?Question 10