naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 2

Mbona Timina hakutaka kumeza tembe?

From Kiswahili — Revision Paper 3 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.

Timina: Mama mimi sitaki dawa.
Mama: Timina dawa ndizo zitakusaidia upone.
Timina: Lakini mama najihisi nimepona.
Mama: Kujihisi ni tofauti na kupona. Ili upone na malaria itoke mwilini, lazima ukamilishe dawa zote ulizopewa na daktari.
Timina: Mama lakini...
Mama: (akimkata kauli): Hakuna cha lakini hapa, shika tembe hizi umeze kisha unywe uji.
Timina: Mama unajua sipendi uji, nitakunywa sharubati.
Mama: Uji ndiyo itakusaidia kuwa na nguvu.
Timina: Mama, Daktari Pendo hakusema hivyo.
Mama: Kazi ya daktari ni kukupima na kukupa dawa, ni jukumu langu kama mama kuhakikisha umemeza dawa na umekula vyema ili kuwa na nguvu.

Mbona Timina hakutaka kumeza tembe?

  1. AAlikuwa anajihisi mgonjwa.
  2. BAlikuwa anajihisi amepona.
  3. CMama yake alikuwa anamlazimisha.
  4. DAlikuwa amepona.

Answer

B. Alikuwa anajihisi amepona.

Timina anasema, "Lakini mama najihisi nimepona." Mama anamweleza kwamba kujihisi ni tofauti na kupona kweli.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test