CBC Grade 2 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 6
SEHEMU B: KUSOMA KWA SAUTI Soma hadithi ifuatayo kwa sauti.
From Kiswahili — Term 1 Assessment 2025 (Set 4) · 20 marks · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Sauti
Mama amevaa rinda la rangi nyekundu. Yeye anapenda rangi nyekundu. Amevaa viatu vinavyometameta. Anapendeza sana. Kila siku ya Jumapili sisi huhudhuria ibada kanisani. Huwa tunavaa mavazi yetu yanayopendeza.
SEHEMU B: KUSOMA KWA SAUTI
Soma hadithi ifuatayo kwa sauti.
Answer
Leo ni siku ya Jumapili. Tunajitayarisha kwenda kanisani na watu wa familia yangu. Nimevaa mavazi ya rangi ya samawati na shati jeupe. Nimevalia soksi za rangi nyeusi. Mama yangu anataka nivae viatu vyangu vipya. Baba ndiye alininulia viatu hivyo. Baba amevaa suruali ndefu na shati ambalo ni ya rangi sawa na yangu. Amejifunga tai shingoni. Mimi na baba tumevaa mavazi yanayofanana. Mama amevaa rinda la rangi nyekundu. Yeye anapenda rangi nyekundu. Amevaa viatu vinavyometameta. Anapendeza sana. Kila siku ya Jumapili sisi huhudhuria ibada kanisani. Huwa tunavaa mavazi yetu yanayopendeza.
Soma kila neno wazi na usimame kwenye kitone. Tamka vizuri maneno kama tunajitayarisha, samawati, alininulia, vinavyometameta na huhudhuria.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.