naQonda

CBC Grade 2 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 10

Watu hujiandaa kwa kufanya nini?

From Kiswahili — CBC Assessment 2025 (Set 1) · 2 marks · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

Watu husherehekea Krismasi dunia nzima. Krismasi ni sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa Yesu. Wakristo ndio wanaoisherehekea. Watu wengi husafiri kutoka jijini kwenda vijijini. Wanakutana na familia zao zote. Wengine hujiandaa kwa kusonga nywele, kununua nguo mpya na kununua vyakula. Watoto ndio huwa na furaha zaidi. Siku hii kuu huwa tarehe ishirini na tano mwezi wa Disemba. Makanisa, maduka makubwa na nyumba hupambwa kwa ajili ya sikukuu hiyo ya Krismasi. Miti hupambwa na mishumaa, kengele na zawadi ndogo. Watoto mara nyingi huenda makanisani ili kusoma mashairi kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo na pia kucheza ngoma. Chakula huandaliwa jioni. Watu wengi huchinja kondoo, kuku, ng'ombe au mbuzi. Watu wengi pia hula pilau au wali na ugali.

8. Watu hujiandaa kwa kufanya nini?

Answer

Kusonga nywele na kununua nguo mpya.

Wengine hujiandaa kwa kusonga nywele, kununua nguo mpya na kununua vyakula.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 2 Kiswahili questions from this test