CBC Grade 9 Kiswahili Exam Term 3 · Question 1
Ni nani aliyekuwa akimtesa Vumilia?
From Test 112 — Kazi ya Ziada (Kiswahili) · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1 hadi 7.
Baada ya mateso ya muda mrefu kwenye mkono wa mwajiri katili, Vumilia alinyanyuliwa na maafisa wa serikali waliosimamia haki za watoto. Mwajiri wake alijikuta mashakani alipopatikana akimtesa. Siku hiyo kweli ilikuwa siku ya afua kwa Vumilia. Mwajiri alishikwa na askari na kupelekwa ndani.
Vumilia alipelekwa shuleni aendelee na masomo yake. Kweli liandikwalo na Mungu lazima liwe. Naye Vumilia alisoma hadi kilele cha masomo hata ingawa alikuwa maskini hohehahe. Alikwenda chuoni kusomea urubani, baadaye aliajiriwa kazi na shirika la ndege la Kenya. Hapo aliweza kupata pesa nzuri kwa mahitaji yake.
Huko nyumbani wazazi wake waliendelea kudhoofika kimaisha waliposikia kuwa mtoto wao wa pekee kapata kazi wingu la tamaa liliwajia. Ajabu lakini ni kuwa wingu hilo halikuwa mvua ya mafuriko kwao. Vumilia aliponda mali na kutia maskio nta. Ama kwa hakika mirija yao ilivukuta uhondo wa kutosha kutokana kwa mwanzao waliogelea kwenye mavuno ambayo hawakuyapalilia wala kunyunyizia maji.
Kwa bahati mbaya, kutokana na makosa madogo Vumilia alifutwa kazi hapo ndipo marafiki wote walipomtoroka. Wazazi wake waliposikia hivyo walikwenda kumtafuta wakaishi naye hadi akapata ajira nyingine.

Answer
Mwajiri wake.
Angalia mwongozo wa kusahishi/kigezo cha alama.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- Eleza maana ya maelezo 'liandikwalo na Mungu lazima liwe'.Question 2
- Kulingana na kifungu ulichokisoma mwanzoni Vumilia alinyimwa haki gani?Question 3
- Kwa nini marafiki walimtoroka Vumilia?Question 4
- Taja sifa mbili za wazazi wake Vumilia kulingana na kifungu ulichokisoma.Question 5
- Ni nini maana ya kutia maskio nta?Question 6
- Ni nini si sahihi kulingana na habari uliyosoma?Question 7