naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 8

Andika sifa tatu zinazotambulisha kifungu hiki kama tamthilia. (Alama 3)

From Test 89 — K.J.S.E.A Kiswahili Karatasi ya 2, Muhula 2 Tathmini ya Mwisho 2026 · 3 marks · Topic: Fasihi, Tamthilia

Dondoo la Tamthilia
Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali yanayofuata.

(Mapema asubuhi nyumbani kwake Mabula)

Mabula: Mbona hivyo?
Mishi: Hamna kitu, nimeshangaa tu.
Mabula: Umeshangaa nini?
Mishi: (Kwa upole) Kumbe umekonda kama ng'onda mume wangu. Hata suti hii iliyokuwa inakuchukua vizuri sasa inakupwaya. (Kwa uchungu) Haidhuru. Hivyo walivyokutenda. Mungu atakulipa.
Mabula: (Anacheka kwa muda) Lahaula!
Mishi: Je, kuna nini?
Mabula: Kwake Dama mimi ninaona tofauti kabisa. Siku zile Dama alikuwa mtoto tunaweza kumwita softie, yaani mlegevu katika mambo mengi. Unakumbuka alikuwa hawezi kuchambua mchele? Unakumbuka alikuwa hawezi hata kukata kucha zake mwenyewe? Unakumbuka alikuwa hawezi kucheza na wenzake? (Kimya) Alikuwa mvivu wa kujituma kufanya kazi. Michezo yake ilikuwa ya kompyuta, burudani yake ilikuwa televisheni. Alikuwa mnyonge. (Kwa msisitizo) Hakuwa mbunifu. Na wewe hukutaka afanye lolote kwa kuwa ulitaka kila jambo lifanywe na yeye kwa kuwa analipwa.

Andika sifa tatu zinazotambulisha kifungu hiki kama tamthilia. (Alama 3)

Answer

Kuna majina ya wahusika (Mabula na Mishi).; Kuna mazungumzo ya moja kwa moja.; Kuna maelekezo ya jukwaa kama (Mapema asubuhi nyumbani kwake Mabula) na (Kwa upole)..

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test