CBC Grade 9 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 11
Jadili mfano mmoja wa maudhui yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)
From Test 89 — K.J.S.E.A Kiswahili Karatasi ya 2, Muhula 2 Tathmini ya Mwisho 2026 · 2 marks · Topic: Fasihi, Tamthilia
Dondoo la Tamthilia
Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali yanayofuata.
(Mapema asubuhi nyumbani kwake Mabula)
Mabula: Mbona hivyo?
Mishi: Hamna kitu, nimeshangaa tu.
Mabula: Umeshangaa nini?
Mishi: (Kwa upole) Kumbe umekonda kama ng'onda mume wangu. Hata suti hii iliyokuwa inakuchukua vizuri sasa inakupwaya. (Kwa uchungu) Haidhuru. Hivyo walivyokutenda. Mungu atakulipa.
Mabula: (Anacheka kwa muda) Lahaula!
Mishi: Je, kuna nini?
Mabula: Kwake Dama mimi ninaona tofauti kabisa. Siku zile Dama alikuwa mtoto tunaweza kumwita softie, yaani mlegevu katika mambo mengi. Unakumbuka alikuwa hawezi kuchambua mchele? Unakumbuka alikuwa hawezi hata kukata kucha zake mwenyewe? Unakumbuka alikuwa hawezi kucheza na wenzake? (Kimya) Alikuwa mvivu wa kujituma kufanya kazi. Michezo yake ilikuwa ya kompyuta, burudani yake ilikuwa televisheni. Alikuwa mnyonge. (Kwa msisitizo) Hakuwa mbunifu. Na wewe hukutaka afanye lolote kwa kuwa ulitaka kila jambo lifanywe na yeye kwa kuwa analipwa.

Answer
Malezi — Mishi anamlea Dama kwa kumfanyia kila jambo, jambo ambalo limemfanya kuwa mvivu na kutokujitegemea..
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- Huku ukitolea mifano, taja tamathali mbili za lugha ambazo zinajitokeza katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)Question 12
- Shairi la aina hii huitwaje? (Alama 1)Question 13
- Taja kibwagizo cha shairi hili. (Alama 1)Question 14
- Kina cha kati katika beti ya tatu ni kipi? (Alama 1)Question 15
- Andika mleo wa ubeti wa nne. (Alama 1)Question 16
- Shairi hili linahusu nini? (Alama 1)Question 17