naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 17

Shairi hili linahusu nini? (Alama 1)

From Test 89 — K.J.S.E.A Kiswahili Karatasi ya 2, Muhula 2 Tathmini ya Mwisho 2026 · 1 mark · Topic: Fasihi, Ushairi

Shairi
Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata.

Miradi tuifanyeni, mizuri na ya riziki
Kwa wengi tujifunzeni, makundi tuyahakiki
Ndege tufuge nyumbani, daima tuipe tiki
Akiba kwetu ni mali, ambayo hayataoza

Akiba kwa elimu, hii kwetu ni muhimu
Kwetu sisi ni jukumu, kwa vitabu na kalamu
Baadaye tuje jikimu, kwa hela sizo haramu
Akiba kwetu ni mali, ambayo hayataoza

Kupitia kwa sanaa, tukuze na uchoraji
Tushone kwayo miyaa, tusifute hadi jiji
Kipaji chetu angaa, tutunze sisi magwiji
Akiba kwetu ni mali, ambayo hayataoza

Bidii na darasani, uwe ni wetu wajibu
Tuifanye kwa makini, sawa yakawe majibu
Tuepuke na uhuni, tuwe badaye tabibu
Akiba kwetu ni mali, ambayo hayataoza

Wosia nimeshatoa, wazazi ninagura
Tangu mpate pokea, mjitolee kwa hasara
Hakika kayapakua, msiiweke hasira
Akiba kwetu ni mali, ambayo hayataoza

Shairi hili linahusu nini? (Alama 1)

Answer

Umuhimu wa akiba, bidii, elimu na matumizi bora ya vipaji katika maisha..

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test