CBC Grade 9 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 4
(c) Eleza maana ya: “Ahadi hizo zilibaki katika mawazo yake tu.” (Alama 1)
From Test 89 — K.J.S.E.A Kiswahili Karatasi ya 2, Muhula 2 Tathmini ya Mwisho 2026 · 1 mark · Topic: Fasihi, Fasihi Simulizi
Hadithi ya Sungura na Fisi
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Sungura na fisi walikuwa majirani. Walishiriki shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji wa wanyama na uuzaji wa mazao sokoni. Kati yao, sungura ndiye aliyejaliwa akili zaidi ndani ya kichwa chake kidogo. Mara kwa mara alimdhulumu mwenzake kwa lengo la kujifaidi au kumtia mwenzake taabani. Kila mara haya yalipofanyika, fisi alijishika sikio akajiahidi kwamba angeachana na rafiki huyo ndumakuwili na kutumia akili yake zaidi. Hata hivyo ahadi hizo zilibaki katika mawazo yake tu.
Siku moja, fisi na sungura walienda kuuza mazao kama ilivyokuwa ada yao. Biashara ilikuwa nzuri tangu asubuhi. Ilipofika jioni walikuwa na vitita vya pesa. Walinunua vitu vichache na kufunga safari kurudi nyumbani.
Walipofika kwenye kichaka kikubwa, sungura alijidai kwenda kujisaidia. Alichukua kofia kubwa, kabuti na miwani mieusi. Kisha alimshambulia fisi kwa fimbo. Fisi alipiga mayowe lakini sungura alimnyang'anya pesa zote na kutoweka.

Answer
Fisi hakutekeleza ahadi zake; aliwaza tu bila kuchukua hatua..
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- (d) Taja sifa mbili za sungura. (Alama 2)Question 5
- (e) Taja mbinu tatu za lugha zilizotumika katika hadithi hii. (Alama 3)Question 6
- (f) Fafanua funzo moja. (Alama 1)Question 7
- Andika sifa tatu zinazotambulisha kifungu hiki kama tamthilia. (Alama 3)Question 8
- Eleza mandhari yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 1)Question 9
- Bainisha matumizi mawili ya maelekezo ya jukwaa kwa kurejelea sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)Question 10