naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 4

Toa neno lingine lenye maana sawa na neno “kiri”.

From Test 6 — Term 2: Endterm Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Msamiati

Mazungumzo kati ya Chifu na Mapunda
(Mapunda amefikishwa kwa Chifu akiwa amefungwa mikononi kwa kosa la wizi. Ni asubuhi na kikundi cha watu kimeketi nje ya ofisi ya Chifu.)
Chifu: Hujambo Mapunda? Mbona unaonekana na wasiwasi?
Mapunda: (Kwa woga) Mimi ni mzima na sina wasiwasi, Bwana Chifu.
Chifu: (Kwa tabasamu) Waona sasa! Umejibu salamu visivyo. Unajua kwa nini umefikishwa hapa?
Mapunda: (Akisitasita) Si… sina ufahamu, Bwana Chifu.
Chifu: Umefikishwa hapa kwa kosa la kuiba kuku wa jirani yako, Mariasa.
Mapunda: Namwomba msamaha. Wanangu walinisumbua sana wakitaka kula kitoweo cha nyama. Uchu wa kula nyama ukanisukuma kumuiba kuku wa jirani.
Chifu: Wazee pamoja na Mariasa wameamua kukusamehe kwa sharti moja: umnunulie kuku mwenye umbo na uzani sawa na yule uliyemwiba.

Toa neno lingine lenye maana sawa na neno “kiri”.

Answer

Kukubali.

Neno "kiri" (kukiri) humaanisha kukubali kuwa umetenda kosa. Maneno mengine yenye maana sawa ni "kukubali" na "kuungama". Kumbuka: "kukiri" ni neno lilelile, kwa hivyo si "neno lingine"; swali linataka neno tofauti lenye maana sawa.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test