naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili End Term 2 Exam 2026 · Question 8

Neno “soni” lina maana gani katika shairi hili?

From Test 6 — Term 2: Endterm Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ushairi

Shairi
Mtumai cha nduguye, kisha hufa masikini,
Kamwe hana apendaye, muunge kiujirani,
Sisahau aombaye, si siri haoni soni,
Ajizi hakika jua, daima nyumba ya njaa.

Usingizi sio mali, amka uende kazi,
Usijiunge na hali, ya kudai hujiwezi,
Jamani usikubali, kulala ukibarizi,
Ajizi hakika jua, daima nyumba ya njaa.

Neno “soni” lina maana gani katika shairi hili?

Answer

Aibu (haya).

"Soni" ni aibu au haya. Mstari "si siri haoni soni" unamaanisha kwamba mvivu anayeomba kila wakati haoni aibu. Neno hili pia hutumika katika msemo "kukosa soni" (kukosa aibu).

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test