CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 3 · Question 18
(b) Ni wahusika gani wanashauriwa katika shairi hili? (alama 1)
From Test 83 — Kiswahili Paper 2 Opener Term 3 · 1 mark · Topic: Fasihi, Ushairi
ZOEZI V: USHAIRI (Alama 5)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
KAMA HAO
Na Elvis Alukwe
Wenzenu tu jukwaani, na huzuni chungu nzima
Fununu zipo hewani, chetu kizazi si wima
Eti wale wa zamani, tabia likuwa njema
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Yao lugha ilifana, nzuri yenye itikadi
Lugha va heshima sana, Kiswahili walinadi
Na hawakutukanana, lugha mufti ilizidi
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Wenye umoja shuleni, kwa pamoja lishikana
Hata mgonjwa kwa bweni, lisaidiwa bayana
Na mwanafunzi mgeni, lisaidika kwa sana
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Nguo nadhifu livaa, vyema walijisitiri
Shuleni na waling'aa, usafi walihubiri
Hawakuvaa mawaa, zao sare lishamiri
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Mefika wakati wetu, wanasema twenda kombo
Tabia mekuwa mwitu, twazamisha chetu chombo
Maadili tele kutu, twachafua yetu nembo
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Ni wapi tuliteleza, kizazi kikapotoka?
Walimu tunawabeza, jamii imetuchoka
Ni sisi twajiumiza, tujaribu rekebika
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Hizi fununu zikome, wanafunzi tuamke
Tusafishe zetu ngome, walimu tuwapulike
Maadili tusichome, kizazi kisianguke
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
KAMA HAO
Na Elvis Alukwe
Wenzenu tu jukwaani, na huzuni chungu nzima
Fununu zipo hewani, chetu kizazi si wima
Eti wale wa zamani, tabia likuwa njema
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Yao lugha ilifana, nzuri yenye itikadi
Lugha va heshima sana, Kiswahili walinadi
Na hawakutukanana, lugha mufti ilizidi
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Wenye umoja shuleni, kwa pamoja lishikana
Hata mgonjwa kwa bweni, lisaidiwa bayana
Na mwanafunzi mgeni, lisaidika kwa sana
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Nguo nadhifu livaa, vyema walijisitiri
Shuleni na waling'aa, usafi walihubiri
Hawakuvaa mawaa, zao sare lishamiri
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Mefika wakati wetu, wanasema twenda kombo
Tabia mekuwa mwitu, twazamisha chetu chombo
Maadili tele kutu, twachafua yetu nembo
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Ni wapi tuliteleza, kizazi kikapotoka?
Walimu tunawabeza, jamii imetuchoka
Ni sisi twajiumiza, tujaribu rekebika
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
Hizi fununu zikome, wanafunzi tuamke
Tusafishe zetu ngome, walimu tuwapulike
Maadili tusichome, kizazi kisianguke
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?
(b) Ni wahusika gani wanashauriwa katika shairi hili? (alama 1)
Answer
Wanafunzi/Kizazi cha sasa.
Angalia jibu la mfano na vigezo vya alama hapo juu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- (c) Bainisha mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika ubeti wa kwanza. (alama 2)Question 19
- ZOEZI I: INSHA (Alama 15) 1. Andika insha kuhusu umuhimu wa kusoma vitabu na jinsi vitabu vimekuwa chanzo cha maarifa…Question 1
- (a) Kipera cha hadithi hii ni nini? Toa sababu moja kuthibitisha jibu lako. (alama 2)Question 2
- (b) Eleza sifa mbili za Neema kama zinavyojitokeza katika hadithi hii. (alama 2)Question 3
- (c) Ni ujumbe gani mkuu unapatikana katika hadithi hii? (alama 1)Question 4
- (d) Taja mandhari mbili tofauti zinazojitokeza katika hadithi hii. (alama 2)Question 5