naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 3 · Question 17

(a) Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 2)

From Test 83 — Kiswahili Paper 2 Opener Term 3 · 2 marks · Topic: Fasihi, Ushairi

ZOEZI V: USHAIRI (Alama 5)

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

KAMA HAO
Na Elvis Alukwe

Wenzenu tu jukwaani, na huzuni chungu nzima
Fununu zipo hewani, chetu kizazi si wima
Eti wale wa zamani, tabia likuwa njema
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?

Yao lugha ilifana, nzuri yenye itikadi
Lugha va heshima sana, Kiswahili walinadi
Na hawakutukanana, lugha mufti ilizidi
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?

Wenye umoja shuleni, kwa pamoja lishikana
Hata mgonjwa kwa bweni, lisaidiwa bayana
Na mwanafunzi mgeni, lisaidika kwa sana
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?

Nguo nadhifu livaa, vyema walijisitiri
Shuleni na waling'aa, usafi walihubiri
Hawakuvaa mawaa, zao sare lishamiri
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?

Mefika wakati wetu, wanasema twenda kombo
Tabia mekuwa mwitu, twazamisha chetu chombo
Maadili tele kutu, twachafua yetu nembo
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?

Ni wapi tuliteleza, kizazi kikapotoka?
Walimu tunawabeza, jamii imetuchoka
Ni sisi twajiumiza, tujaribu rekebika
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?

Hizi fununu zikome, wanafunzi tuamke
Tusafishe zetu ngome, walimu tuwapulike
Maadili tusichome, kizazi kisianguke
Jamii yajiuliza, wako wapi kama hao?

(a) Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 2)

Answer

Ujumbe mkuu ni kutaka kizazi cha sasa kirejelee maadili mema na tabia njema zilizokuwa zikifuatwa na vizazi vya zamani — kuhimiza umuhimu wa lugha ya heshima, umoja, usafi, na kujitahidi kurekebisha tabia mbaya ili kujenga mustakabali bora.

Angalia jibu la mfano na vigezo vya alama hapo juu.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test