naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili School Based Assessment 2025 · Question 23

Faida ipi ya kupanga muda imetajwa?

From Kiswahili — KJSEA Assessment 2025, Code 011 (Set 16) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Mazungumzo

KIFUNGU CHA TANO: MAZUNGUMZO (Maswali 21–24)
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.

Mwalimu: Leo tunajadili umuhimu wa muda. Nani anaweza kueleza maana ya kupangilia muda vizuri?

Jane: Mwalimu, kupangilia muda hutusaidia kumaliza kazi bila haraka haraka.

Mwalimu: (21) ______ sana Jane. Je, kuna faida nyingine?

Ali: Ndiyo Mwalimu. Hupunguza msongo wa mawazo na kutufanya tufanye mambo kwa utaratibu.

Mwalimu: Huo ni ukweli. Kuna changamoto gani katika kupanga muda?

Peter: Wanafunzi wengine hupoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii.

Mwalimu: (22) ______, Peter. Hilo ni tatizo kubwa. Tukiwa na nidhamu, tunaweza kutumia muda vizuri.

23. Faida ipi ya kupanga muda imetajwa?

  1. AKuongeza usingizi
  2. BKumaliza kazi kwa haraka haraka
  3. CKupunguza msongo wa mawazo
  4. DKuchelewesha kazi

Answer

C. Kupunguza msongo wa mawazo

Ali anasema kupanga muda hupunguza msongo wa mawazo. Jane alisema husaidia kumaliza kazi bila haraka haraka, si kwa haraka haraka.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test