naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 10

Kama wewe ni kiongozi wa vijana katika mtaa wako, ni hatua gani kati ya hizi utachukua ili kutekeleza pendekezo la mwandishi?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 5) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 8 hadi la 11.
Ni jambo la kusikitisha na linalokata ini kuona jinsi vijana wetu, ambao ni nguzo na uti wa mgongo wa taifa, wanavyotumbukia katika lindi la kiza la matumizi na uuzaji wa mihadarati. Badala ya kuwa mstari wa mbele kuijenga nchi kama ilivyotarajiwa, wengi wameanza kuwa kama mshumaa unaowaka pande zote mbili-wanateketea upesi huku nuru yao ikizimika kabla ya kuchanua.
Mihadarati imepenya miongoni mwa vijana hawa kama moshi uingiao kwenye nyufa, ikichochewa na ukata na uhaba wa ajira unaowafanya kukata tamaa na kupoteza mwelekeo. Inasikitisha kuwa hali hii imekuwa fursa kwa baadhi ya mabwenyenye walafi ambao ni mbwa mwitu waliovalia ngozi ya kondoo. Mabwenyenye hawa huwatumia vijana kama mawakala wa biashara zao haramu, wakijitajirisha kwa kutoa kafara mustakabali wa kizazi kijacho.
Kwa hakika, vijana ni chemchemi ya matumaini na rasilimali muhimu kwa jamii yoyote. Kuruhusu wapotelee katika uraibu huu ni sawa na kuyaruhusu maua ya nchi yanyauke mchangani. Ni lazima kila mzalendo ajifunge kibwebwe kuhakikisha kuwa vijana hawa hawaponyoki mikononi mwa jamii na kutumbukia katika mitego hiyo ya mauti.
Ili kuwakomboa, hatuna budi kuwanoa kiakili kwa mafunzo, kuwatengenezea nafasi za ajira, na kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali za kijamii. Tukifanya hivi, tutakuwa tumeuziba ufa kabla ya kujenga ukuta, kwani kinga ni bora kuliko tiba, na taifa lisilo na vijana wenye maadili ni sawa na jahazi lililopoteza dira katikati ya bahari kuu.

10. Kama wewe ni kiongozi wa vijana katika mtaa wako, ni hatua gani kati ya hizi utachukua ili kutekeleza pendekezo la mwandishi?

  1. AKuwatafutia vijana wenzako mawakala wa biashara za siri.
  2. BKuandaa mashindano ya michezo na warsha za mafunzo ya kazi.
  3. CKuwahimiza vijana wajifunze jinsi ya kuwaka kama mshumaa.
  4. DKuwaomba mabwenyenye watoe pesa za bure kwa vijana.

Answer

B. Kuandaa mashindano ya michezo na warsha za mafunzo ya kazi.

Mwandishi anapendekeza mafunzo na kuwashirikisha katika shughuli za kijamii.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test