CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5
Chagua kauli sahihi kulingana na taarifa uliyosoma
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma habari ifuatayo kisha ujibu swali la 1 - 10.
Dunia imejaa mikasa na visa tumbi. Navyo ni vingi havihesabiki. Ni lukuki. Naam, visa na mikasa mzomzo. Bila shaka, kwa mintarafu hii ndipo wahenga na wahonguzi wakasanifu na kusharifu msemo, "Baada ya kisa mkasa." Naam, yote haya ni malimwengu ulimwenguni.
Katika uo huo mkururo wa visa na mikasa ambavyo vikitukia hugonga vichwa vya habari katika vyombo mbalimbali vya mawasiliano kama vile: redio, runinga, magazeti, majarida na vinginevyo. Mikasa mingine hudumu sana katika marejeleo ya upashanaji habari ambapo mingine huyeyuka harakaharaka kama vibongo vya barafu na kutokomea katika hewa yabisi. Ama tuseme, huzikwa katika makaburi ya sahau za fika za mahuluki.
Ndugu wapenzi, visa ni vingi na mikasa ni mingi. Vipo visa vinavyoudhi na kukora mno. Vingine havikeri tu mbali pia husangaza na kumwacha mtu mwadilifu kinywa wazi akimaka, "Lo. salaala! Kuna nini! Au hizi ndizo zama zile za miti kusema na nyani kuvaa miwani? Ama ndizo enzi za samaki kuhama majini na kuhamia nchi kavu? Vipi visa hivi? Ebo! Afanalek! Tumefika kiama ama nini? Ujambazi, wizi, ulevi, mihadarati, ukwaro, hongo, ajali, mizozo, chuki, unyama na ubakaji peupe peupe ni tuwazimu wa mizuka iliyozuka kutoka wapi? Ndugu wapendwa wazalendo tusipoyastaajabu haya tutapata haya. Asiye haya ni hayawani. Kuna kisingizo gani katika kuendeleza visa na mikasa sampuli hii? Pukachaka. Tokezeni tuyalaani majanga haya kwa pamoja. Semeni, uhayawani zii?"
Licha ya hayo machafuko ya matendo, leo mnamo tarehe tisa mwezi wa kumi na moja mwaka wa elfu mbili na nne, siku ya kwanza ya mitihani wa wanafunzi wa gredi ya nane nchini. Vyombo vya habari nchini vimetangaza kifo cha mwanafunzi wa gredi ya saba aliyeanguka kutoka kwenye mti na kubwagika chini pu! maiti! makubwa haya! Taarifa za kuaminika katika duru za vyombo vya habari zinasema kwamba, Bwana mdogo huyo mwenye umri wa miaka kumi na minne aliamriwa na mwalimu wake akakweo mti ili akate fimbo au ufito wa kuenda kumwadhibia kijana mwenyewe. Ala! potolea pote, hata kama alikosa vipi, ndipo yeye mwenyewe yuyo huyo mkosaji ajinolee kisu cha kumdungia.
Aisee! Haki za watoto ziko wapi? Au ndiyo hii inayotekelezwa kwa fito? Chondo chode wananchi na walimu wazalendo, tuwapende watoto, tuwatunze na kuwalinda. Tukiwaua, tutafundisha kina nani? Hata hivyo nanyi watoto mkitetewa mjaribu kutii. Elimu ni yenyu.
5. Chagua kauli sahihi kulingana na taarifa uliyosoma
- Amatendo maovu na visa vilivyotajwa hapa havifai kutokea hata kidogo katika taifa la kizalendo.
- Bvisa hivi vya kuudhi labda vingefaa vitokee tu wakati wa kiama wala si katika jamii.
- Cvitendo viovu ni sehemu ya maisha kwa hivyo tuvumilie tu.
- Dlazima kila mmoja wetu aliye wadilifu ayalaani matendo maovu yanapotokea
Answer
A. matendo maovu na visa vilivyotajwa hapa havifai kutokea hata kidogo katika taifa la kizalendo.
Mwandishi anasema visa hivi havina kisingizo katika jamii ya wazalendo, na anatuhimiza tuyalaani pamoja.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Mwandishi hasemi kwambaQuestion 6
- Tunaarifiwa kwamba kisa cha hivi karibuni kabisa cha mkasa niQuestion 7
- Mwalimu alipomwamuru Bwana Mdogo akakate fimbo alidhamiria nini?Question 8
- Hatua aliyochukua mwalimu ya kumwadhibu kijana huyo kwa fimboQuestion 9
- Taarifa hii inazingatia na kutetea maswala yaQuestion 10
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi 11.Question 11