naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 1

Taarifa hii inatudokezea kwamba mikasa imejaa na kuzidi kuongezeka kwa sababu

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma habari ifuatayo kisha ujibu swali la 1 - 10.
Dunia imejaa mikasa na visa tumbi. Navyo ni vingi havihesabiki. Ni lukuki. Naam, visa na mikasa mzomzo. Bila shaka, kwa mintarafu hii ndipo wahenga na wahonguzi wakasanifu na kusharifu msemo, "Baada ya kisa mkasa." Naam, yote haya ni malimwengu ulimwenguni.

Katika uo huo mkururo wa visa na mikasa ambavyo vikitukia hugonga vichwa vya habari katika vyombo mbalimbali vya mawasiliano kama vile: redio, runinga, magazeti, majarida na vinginevyo. Mikasa mingine hudumu sana katika marejeleo ya upashanaji habari ambapo mingine huyeyuka harakaharaka kama vibongo vya barafu na kutokomea katika hewa yabisi. Ama tuseme, huzikwa katika makaburi ya sahau za fika za mahuluki.

Ndugu wapenzi, visa ni vingi na mikasa ni mingi. Vipo visa vinavyoudhi na kukora mno. Vingine havikeri tu mbali pia husangaza na kumwacha mtu mwadilifu kinywa wazi akimaka, "Lo. salaala! Kuna nini! Au hizi ndizo zama zile za miti kusema na nyani kuvaa miwani? Ama ndizo enzi za samaki kuhama majini na kuhamia nchi kavu? Vipi visa hivi? Ebo! Afanalek! Tumefika kiama ama nini? Ujambazi, wizi, ulevi, mihadarati, ukwaro, hongo, ajali, mizozo, chuki, unyama na ubakaji peupe peupe ni tuwazimu wa mizuka iliyozuka kutoka wapi? Ndugu wapendwa wazalendo tusipoyastaajabu haya tutapata haya. Asiye haya ni hayawani. Kuna kisingizo gani katika kuendeleza visa na mikasa sampuli hii? Pukachaka. Tokezeni tuyalaani majanga haya kwa pamoja. Semeni, uhayawani zii?"

Licha ya hayo machafuko ya matendo, leo mnamo tarehe tisa mwezi wa kumi na moja mwaka wa elfu mbili na nne, siku ya kwanza ya mitihani wa wanafunzi wa gredi ya nane nchini. Vyombo vya habari nchini vimetangaza kifo cha mwanafunzi wa gredi ya saba aliyeanguka kutoka kwenye mti na kubwagika chini pu! maiti! makubwa haya! Taarifa za kuaminika katika duru za vyombo vya habari zinasema kwamba, Bwana mdogo huyo mwenye umri wa miaka kumi na minne aliamriwa na mwalimu wake akakweo mti ili akate fimbo au ufito wa kuenda kumwadhibia kijana mwenyewe. Ala! potolea pote, hata kama alikosa vipi, ndipo yeye mwenyewe yuyo huyo mkosaji ajinolee kisu cha kumdungia.

Aisee! Haki za watoto ziko wapi? Au ndiyo hii inayotekelezwa kwa fito? Chondo chode wananchi na walimu wazalendo, tuwapende watoto, tuwatunze na kuwalinda. Tukiwaua, tutafundisha kina nani? Hata hivyo nanyi watoto mkitetewa mjaribu kutii. Elimu ni yenyu.

1. Taarifa hii inatudokezea kwamba mikasa imejaa na kuzidi kuongezeka kwa sababu

  1. Akila kisa huzua mkasa
  2. Bmikasa haihesabiki
  3. Cni mingi
  4. Dwahenga walitetea msemo wao

Answer

A. kila kisa huzua mkasa

Msemo "Baada ya kisa mkasa" unaonyesha kwamba kila kisa huzaa mkasa mwingine.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test