CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 19
d) Ujumbe wa shairi ni upi? (Alama 1)
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 1 mark · Topic: Fasihi, Ujumbe
ZOEZI LA 5: USHAIRI (Alama 5)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
MWANANGU WACHA UOGA
Mashujaa wa uhuru, walijawa ujasiri,
Waliimwaga damu, wakoloni ‘lipajiri,
‘Wakuogopa mitutu, minajili ukombozi,
Mwanangu acha uoga, utimize ndoto zako.
Tazama simba wa nyika, si mrefu njoringori,
Si mjanja ya sungura, si mkali kama ngiri,
Ila wote huwauwa, kwa sababu ni jasiri,
Mwanangu acha uoga, utimize ndoto zako.
Nanasi ni tunda tamu, lamea kati mibani,
Hakua nayo ilhamu, na utamu wa asali,
Si chachu kama limau, licha ya kua mibani,
Mwanangu acha uoga, utumize ndoto zako.
Ya mazidadi sinayo, nimefika hitimisho,
Yafungue masikio, ondoa mafarakano,
Uoga uupe mgongo, jusuru fumbwa jicho,
Mwanangu acha woga, utumize ndoto zako.
(Mtunzi: Daniel Siwa)
d) Ujumbe wa shairi ni upi? (Alama 1)
Answer
Mtoto aache uoga na awe jasiri ili atimize ndoto zake.
Kiitikio kinabeba ujumbe mkuu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- ZOEZI LA 1: INSHA (Alama 15) Mwandikie rafiki yako barua, ukimweleza umuhimu wa kukienzi na kukitumia kiswahili kama…Question 1
- a) Hii ni aina gani ya hadithi. Eleza (Alama 2)Question 2
- b) Andika sifa za hadithi ya aina hii (Alama 2)Question 3
- c) Ni maudhui gani ambayo yanajitokeza katika hadithi hii (Alama 2)Question 4
- d) Eleza sifa bainifu za Mnana (Alama 2)Question 5
- e) Andika maadili ya hadithi hii (Alama 2)Question 6