naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 6

e) Andika maadili ya hadithi hii (Alama 2)

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 1) · 2 marks · Topic: Fasihi, Maadili

ZOEZI LA 2: FASIHI (Alama 10)
Mulungu ndiye aliyeumba binadamu. Kwa vile Mulungu ni mwema daima aliwaambia malaika wake, “Nisingependa binadamu wawe wakifa kabisa. Ningependa binadamu akifa awe anafufuka.” Basi akawaumba binadamu na kuwaweka katika eneo jingine. Mbali na alikoishi yeye mwenyewe Mulungu.

Karibu na nyumba ya Mulungu, paliishi kinyonga na ndege aitwaye mnana. Katika mlagusano wao na Mulungu, Mulungu aliweza kung’amua kuwa ndege huyo alipenda kutia chumvi maneno na hata kusema mambo kinyume na alivyoambiwa. Akamtambua kuwa kiumbe asiyeweza kuaminiwa. Kwa upande mwingine, kinyonga alikuwa mwadilifu na mwenye busara. Hakusema uongo.

Mulungu alipoona wakati umefika wakumpasha binadamu ujumbe wa uzima alimuita kinyonga na kumuambia, “Nenda katika eneo ambamo nimeweka binadamu. Waambie kuwa yeyote atakaye kufa atafufuka.” Kinyonga alisujudu na kusema, “Ndiye, Mulungu.” Hata hivyo, kinyonga alitembea polepole kama kawaida yake. Mnana alibaki nyumbani kwa Mulungu. Kinyonga akahesabu hatua zake polepole akihofia kuumiza ardhi ya wenyewe. Alipofika alikuwa yu hoi, nguvu zimemwishia. Aliwakuta binadamu wamekusanyika pamoja. Taratibu akaanza kutoa ujumbe wake. “Nime...nime... nimeambiwa.....” lakini hakudiriki kusema aliloambiwa.

Mnana alimwomba Mulungu udhuru wa kuondoka. Mulungu akamridhia naye akaruka moja kwa moja hadi alikoishi binadamu. Alimkuta kinyonga katika harakati zake za kusema ‘nime...nime...nimeambiwa’ huku watu wakingoja kwa matarajio makuu kusikia alichoambiwa. Mnana alipofika, kinyonga alikuwa amechoka kiasi cha kusahau ujumbe wenyewe. Kinyonga alipomwona Mnana akamuuliza “Tuliambiwa nini na Mulungu?” Naye Mnana bila kuchelewa akasema, “Tuliambiwa kuwa binadamu wakifa wataangamia na kudidima kabisa kama mzizi ya mshubiri.” Kinyonga akashana na kusema, ‘lakini .......tuli...tuli...tuliambiwa kwa....kwamba.....binadamu wakifa...wa...wata...watakufa tena.....” Hata hivyo kinyonga alikuwa amechelewa. Watu walikuwa wametawanyika wakaelekea makwao nyuso wameziinamisha.

e) Andika maadili ya hadithi hii (Alama 2)

Answer

Tujihadhari na marafiki waongo, na tutimize majukumu yetu kwa wakati.

Funzo hutokana na kilichowapata binadamu.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test